Wasifu Wetu
Halis Foundation inalenga kusaidia watu wa makundi maalum, wakiwemo watoto, wanawake waliotelekezwa na watoto wao, na wazee hasa wale walioko kwenye vituo vya huduma. Shirika hili litaendesha shughuli zake kwa malengo ya misaada ya kijamii, elimu, na utafiti wa kisayansi pekee.
Shirika litaanzisha vituo vya mafunzo kwa lengo la kuwezesha wanawake maskini na vijana kwa kuwajengea uwezo, kuwapa maarifa ya maendeleo ya biashara na ujasiriamali, pamoja na kubadilisha mitazamo yao kuelekea maendeleo ya kiuchumi kwa ukuaji na ustawi wa maisha yao ya kijamii na kiuchumi.